20,99 €
inkl. MwSt.

Versandfertig in 1-2 Wochen
payback
10 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Wataalamu wa lugha na fasihi na mila za watu mbalimbali wametuzindua juu ya utajiri wa fasihi ya Waswahili. Katika fasihi hiyo, tungo za Kiswahili ndilo jambo lililojitokeza mbele kwa mwanga wenye kunawiri sana. Profesa Ibrahim Noor Shariff amefanya utafiti mkubwa kabla ya kukiandika kitabu hiki. Natija yake ni kuwa yaliyoelezwa humu yametufunulia mengi yaliyokuwa dafina. Tokea 1988 kilipochapishwa kitabu hiki kwa mara ya kwanza kimekuwa ni kitabu cha kukirejelea kwani kinaeleza yale ambayo watungaji wa tungo za Kiswahili, wataalamu, waalimu na wanafunzi wanaotaka kuelewa khabari za tungo huwa…mehr

Produktbeschreibung
Wataalamu wa lugha na fasihi na mila za watu mbalimbali wametuzindua juu ya utajiri wa fasihi ya Waswahili. Katika fasihi hiyo, tungo za Kiswahili ndilo jambo lililojitokeza mbele kwa mwanga wenye kunawiri sana. Profesa Ibrahim Noor Shariff amefanya utafiti mkubwa kabla ya kukiandika kitabu hiki. Natija yake ni kuwa yaliyoelezwa humu yametufunulia mengi yaliyokuwa dafina. Tokea 1988 kilipochapishwa kitabu hiki kwa mara ya kwanza kimekuwa ni kitabu cha kukirejelea kwani kinaeleza yale ambayo watungaji wa tungo za Kiswahili, wataalamu, waalimu na wanafunzi wanaotaka kuelewa khabari za tungo huwa wanakirejelea mara kwa mara ili kupata jawabu za masuala yao. Kitabu hiki kimepangwa vizuri sana kwani kila maudhui yameandikwa chini ya kichwa cha khabari kinachoelezea maudhui yanayofuata. Hali kadhalika, kitabu kina mifano ya tungo za kupigiwa mifano. Yoyote anayetaka kuzungumza khabari za tungo za Waswahili hataweza tena kujadili mengi ya maana iwapo atajinyima fursa ya kusoma yaliyoandikwa katika kitabu hiki cha Tungo Zetu.
Autorenporträt
Profesa Ibrahim Noor Shariff amezaliwa kisiwani Unguja mnamo mwaka wa 1941. Amesoma katika skuli mbalimbali za Unguja na Pemba (Zanzibar). Baada ya kumaliza madarasa ya upili, amesoma masomo ya sanaa katika Chuo Kikuu cha Makerere na kupata shahada ya D.F.A. mwaka wa 1967. Baadaye amesoma katika Chuo Kikuu cha Rutgers, New Jersey, Marekani na kupata shahada ya Udaktari wa Ilimu ya Sanaa 1983. Alisomesha sanaa na Kiswahili katika chuo hichohicho cha Rutgers kuanzia mwaka wa 1970. Mwaka wa 1996 alihamia Oman na kusomesha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Sultan Qaboos mpaka alipostaafu 2019. Profesa Ibrahim ameonesha kazi zake za sanaa mwahala mwingi duniani na ameandika mengi kukhusu Waswahili na fasihi yao.