24,99 €
inkl. MwSt.

Versandfertig in 1-2 Wochen
payback
12 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Swahili translation of the Nobel-prize winning author's 1994 novel Paradise. ¿Mzaliwa wa Afrika ya Mashariki, Yusuf anaondoka kwao kwa ghafla akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Haimjii hata kwa sekunde moja, kwamba atakuwa mbali na wazazi wake kwa muda mrefu, na wala hafikirii kuuliza atarudi lini au kwa nini safari iliandaliwa kwa ghafla kiasi kile. Yusuf anaamini kuwa anamsindikiza Ami Aziz lakini ukweli ni kwamba 'ami' yake ni Mfanyabiashara, tena tajiri mkubwa, na Yusuf amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake. Yusuf anajikuta anasafiri katika miji na vitongoji vingi vingine…mehr

Produktbeschreibung
Swahili translation of the Nobel-prize winning author's 1994 novel Paradise. ¿Mzaliwa wa Afrika ya Mashariki, Yusuf anaondoka kwao kwa ghafla akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Haimjii hata kwa sekunde moja, kwamba atakuwa mbali na wazazi wake kwa muda mrefu, na wala hafikirii kuuliza atarudi lini au kwa nini safari iliandaliwa kwa ghafla kiasi kile. Yusuf anaamini kuwa anamsindikiza Ami Aziz lakini ukweli ni kwamba 'ami' yake ni Mfanyabiashara, tena tajiri mkubwa, na Yusuf amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake. Yusuf anajikuta anasafiri katika miji na vitongoji vingi vingine ambako anakutana na watu wa kila namna. Anabalehe na kukua kwenye dunia inayobadilika kwa kasi kutokana na kuingia kwa ukoloni na udhalimu wake na jamii kuharibika kwa kuvurugwa kwa utamaduni wake. Hii ni tafsiri ya kwanza kwa riwaya za Abdulrazak Gurnah katika lugha ya Kiafrika. Abdulrazak Gurnah ni mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021. Ameandika riwaya kumi ikiwemo hii ya paradise. Gurnah ni Profesa wa Masomo ya Kiingereza na Fasihi za Kikoloni katika Chuo Kikuu cha Kent. Dkt. Ida Hadjivayanis ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masomo ya Kiswahili SOAS, Chuo kikuu cha London. Ametafsiri riwaya kadhaa kwa Kiswahili na Kiingereza.