19,99 €
inkl. MwSt.

Versandfertig in über 4 Wochen
payback
10 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Mureti na Mugiira wanapopata ufadhili wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanafurahi sana. Wanaabiri ndege kwa mara ya kwanza na wanaajabia mengi wanayoyaona katika safari yao hadi Marekani. Lakini maajabu ya kweli yanawasubiri California wanakokwenda kusoma. Mapokezi na mlahaka mwema wanaopata kutoka kwa Profesa Kithaka unatiwa doa na wasichana wawili wa Kimarekani; Mary Anne na Brigit wanaotaka mapenzi ya lazima kutoka kwa Mureti na Mugiira. Mary Anne na Brigit wanafanya mipango ya kuwateka Mureti na Mugiira, kwa bastola au hata kwa mkataba (kama alivyotekwa kijana…mehr

Produktbeschreibung
Mureti na Mugiira wanapopata ufadhili wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanafurahi sana. Wanaabiri ndege kwa mara ya kwanza na wanaajabia mengi wanayoyaona katika safari yao hadi Marekani. Lakini maajabu ya kweli yanawasubiri California wanakokwenda kusoma. Mapokezi na mlahaka mwema wanaopata kutoka kwa Profesa Kithaka unatiwa doa na wasichana wawili wa Kimarekani; Mary Anne na Brigit wanaotaka mapenzi ya lazima kutoka kwa Mureti na Mugiira. Mary Anne na Brigit wanafanya mipango ya kuwateka Mureti na Mugiira, kwa bastola au hata kwa mkataba (kama alivyotekwa kijana mmoja wa Kiafrika aitwaye Mburia, kwa kulazimishwa mkataba wa mapenzi) "... kwa siku nyingi umekuwa ukinidanganya kwamba utanioa mara mjombako atakapokupatia kibali. Sasa chukua hii kalamu na karatasi uandike kwamba utanioa!" Je, Mureti na Mugiira watajinasua katika mtego wa wasichana hawa ili kutimiza ndoto yao ya masomo huko California? Wataweza kurudi Afrika ama watatekwa bakunja na utamaduni mpya wa Wamarekani? Watayaacha masomo watoroke au watafanyaje?